
KUNA, mijadala bado inaendelea kwenye mitandao ya Kijamii, kuhusu Neno CLEAN SHEET, kwenye mchezo wa soka linatumikaje.
.
.
CLEAN SHEET, ni kitendo cha timu nzima kucheza bila ya wavu wao kuguswa , hii mara nyingi wana michezo huwa tunaangalia eneo la safu ya ulinzi. Na ukisema safu ya ulinzi inaanzia goal kipa mabeki wake wa kati wapembeni na kiungo namba cha ulinzi hao wote ni safu ya ulinzi ndo huwa mara nyingi wanahusika sana kwenye clean sheet.
.
.
Kwa sababu wao ndo muda mwingi wanafanya majukumu ya ulinzi kwenye eneo la nyuma kama huna safu bora ya ulinzi maana yake kuna asilimia 70 za kuwa kila mechi unaruhusu mabao zipo timu kibao kupata CLEAN SHEET, kwao ni ngumu sana.Leo nimekumbuka maneno ya kocha Jose Mourinho, aliwahi kusema hivi wakati akiwa kocha wa Inter Milan, kuwa ukiwa na safu bora ya ulinzi utatwaa Ubingwa na alikuwa akimaanisha kitu akafanikiwa kutwaa Ubingwa wa Ulaya mwaka 2010.
.
.
CLEAN SHEET, pia inatumika kwenye kuwafananisha wachezaji kila msimu mfano mzuri labda Virgil Van Djick , amecheza michezo 50 ameruhusu wavu kuguswa mara 7 na amepata CLEAN SHEET, 6 na Puyol, amecheza michezo 50 wavu wake umeguswa mara 9 na amepata CLEAN SHEET, mara 4 je nani bora hapo ni Virgil Van Djick, namba zinambeba 🙌🙌.
.
.
Kaka yangu @alikamwe, anasema hivi CLEAN SHEET, ni ya kipa tu sawa je? Kipa anacheza peke yake ndani?jibu ni hapana. Na pia kusema kiungo hasifiwi CLEAN SHEET, je ukitaka kumfaninisha na Kiungo wa timu pinzani ni lazima utimie kigezo cha CLEAN SHEET, amecheza michezo mangapi safu yake ya ulinzi imeruhusu mabao mangapi na vingine.
.
.
Kipa ndo mchezaji anayepata ile Golden glove, kwa sababu kwa upande wa asimilia 80 anaokoa michomo hatari pale timu yake mabeki wanavo kuwa hawachezi vizuri mfano mzuri mchezo wa Jana wa ligi kuu England kati ya Tottenham dhidi ya Liverpool, kipa wa Paul Diano Tottenham, aliokoa michomo 7 kipindi cha kwanza 🙌.
.
.
✍🏻@azizi_mtambo_15 wa @sokaplace_
Powered by @bikotanzania





#VodacomPremierLeague








