
👉 Chini Chini ya Kapeti ni Kwamba mmoja kati ya Hawa Makocha Wazoefu anaweza kuja kuwa Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga SC ambayo kwasasa ipo chini ya Mwinyi Zahera 🇨🇩… Kazi kwenu Wananchi katika Kutafuta Kocha mpya au kuendelea kumuamini na kumuunga Mkono Papaa Zahera 🙌..
:
✍🏻 Kim Poulsen 🇩🇰 kwa mara ya kwanza alitua Nchini Tanzania April 2011 na kuanza kuinoa timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya Umri wa Miaka 21 hadi Mei mwaka 2012 na kuchukua mikoba mwenzake, Jan Børge Poulsen kwenye kikosi cha Taifa Stars… Alitimuliwa japo wengi hawakupenda kuondoka kwake..
…
✍🏻 Raoul Jean-Pierre Shungu 🇨🇩 kwa mara ya kwanza alitua nchini mwaka 1998 kuja kuwa kocha Mkuu wa Yanga SC, Lakini alitimuliwa mwaka 2000…Katika kipindi chake cha kufanya kazi kwake Yanga, Shungu aliipa Yanga Kombe la Afrika Mashariki na Kati, mwaka 1999 katika fainali zilizofanyika Kampala, Uganda 🇺🇬 na mataji kadhaa ya nyumbani, likiwemo Kombe la FA, Nyerere, Muungano na ubingwa wa Bara.. Aliondoka Yanga baada ya kutofautiana na Mwenyekiti wa klabu hiyo wakati huo, Tarimba Abbas baada ya kusema amekwenda Ufaransa kusoma kozi fupi ya FIFA, lakini aliporudi akaambiwa aonyeshe pasipoti yake kama viza ya nchini humo, akawa anapiga chenga, hivyo akaonekana muongo.. Kilichofuatia, aliyekuwa kocha wa African Sports ya Tanga wakati huo, Charles Boniface Mkwasa akaajiriwa kama Meneja wa timu na Shungu akaondolewa.. Kwa Sasa Shungu bado Ni Kocha Msaidizi wa kwanza wa The Dolphins 🐬 “AS Vita Club” 🇨🇩.
…
✍🏻 Hans Van Der Pluijm 🇳🇱 Kwa mara ya kwanza alitua Nchini Tanzania mwaka 2014 kuja kuwa kocha Mkuu wa Yanga SC, Alipata mafanikio makubwa Mno na timu hiyo ya Wananchi na hilo lipo wazi, Aliiongoza Yanga mpaka 2017 akitwaa Ubingwa wa FA, Mataji ya Ligi Kuu na kuifikisha timu katika hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kisha kuwa Mkurugenzi wa Ufundi kwa muda mfupi kisha kutimka, akatua Singida Kisha kumaliza Career yake Nchini akiwa na Azam FC..
#TransfersNews #VPLUpdates #CAFCC
✍🏻 @Harunlugoyah