Safari ya bale.kwenda china yayeyuk

Wakala wa nyota wa kimataifa wa Wales na klabu ya Real Madrid Gareth Bale bwana Jonathan Barnett amekanusha tetesi za mteja wake kutaka kutimkia China kama inavokaririwa na vyombo kadhaa vya habari.
.
Barnett amesema “Usiamini kila unachokisikia,Bale ana furaha hapa Madrid na hana mpango wowote wa kuondoka klabuni hapa kwa siku za Usoni”.
.
.
Prepared by @anode360 Proudly Sponsored by @mcheza_tz @bussi_ntua @tshombee1 #sokaonlineupdates

GOR Mahia yapata wadhamini wapya

✍🏻 Klabu ya GOR Mahia ya Kenya πŸ‡°πŸ‡ͺ na Kampuni ya Agro Chemical And Food Co Ltd wameingia Mkataba wa Miaka Mitano ya Udhamini, ambapo Kampuni hiyo itaitumia klabu hiyo Kubwa Afrika Mashariki kutangaza bidhaa zao za Vinywaji.

πŸ‘‰ K’Ogalo itanufaika na uuzwaji wa Kilevi cha Patriot Gin Kwa Kipindi chote cha Mkataba, Kwa kila chupa inayouzwa kilabu itapata Kshs 5.
..
✍🏻 Ikumbukwe, Mdhamini wa Klabu hiyo kwa miaka mitatu iliyopita – Sportpesa – imejitoa katika ushirikiano wao miezi minne iliyopita baada ya kampuni hiyo ya betting kusitisha shughuli zake nchini Kenya πŸ‡°πŸ‡ͺ.
#KPL #GORMahia #KenyaPremierLeague
@Harunlugoyah

BREAKING NEWS : Jose Mourinho yupo tayari kwa kuchukua kazi ya Unai Emery.

Hadi sasa habari za chinichini ni kwamba ma-boss wa Arsenal wanaweza kumfukuza kazi Unai Emery.

Swali la nani atachukua mikoba ya Arsenal jina linalotajwa sana ni Jose Mourinho. Kipindi cha television kinachohusu maswala ya soccee wamesema kwamba bodi ya Arsenal ipo sawa kumpa kazi Mourinho.

Upande wa Mourinho napo wapo sawa na kazi ya kuinoa Arsenal kwasababu ndio level ambayo kocha huyo anataka. Aliwai kusema atarudi kuwa kocha lakini kwenye club ya level za juu na sio chini.

Hivi karibuni Mourinho alienda Emirates Stadium kuangalia mechi ya Europa League kati ya Arsenal dhidi ya VItoria.

Mashabiki wa Gunners, Jose Mourinho kama kocha wenu mpya mnaipokea vipi hii.

Arsenal ,Liverpool na Manchester united vitani

Klabu za Arsenal ,Liverpool na Manchester united zimeanza mazungumzo na wawakilishi wa mshambuliaji wa Borrusia Monchengladbach Denis Zakaria ili kuweza kujiunga katika klabu hizo.

Sky German limethibitisha kuwepo kwa mazungumzo kati ya wawakilishi wa Denis na Borrusia na klabu hizo kwa nyakati tofauti.

Mwenye kisu kikali ndiye atakula nyama! Unadhani nani atafanikiwa kumsajili Zakaria!?
.
.
Prepared by @anode360 Proudly Sponsored by @mcheza_tz @bussi_ntua @tshombee1 #sokaonlineupdates

Viwanja kuwaka Liverpool Vs Arsenal carabao cup

Carabao cup|
Liverpool Vs Arsenal|
Saa 2:30.
Uwanja:Anfield,Liverpool.
.
✍Kuelekea Mchezo wa leo wa Carabao Cup recently Liverpool wamekua mwiba si kwa Arsenal tu bali karibu kila timu inayokutana nayo!.
.
✍kwa miaka ya hivi karibuni Arsenal wamekuwa si chochote mbele ya Liverpool’Mabingwa wa Ulaya’!.
.
✍Katika mechi 9 za mwisho Arsenal wamepoteza mechi 5 tena zikiwa na idadi kubwa ya magoli moja kwa .oja takwimu haziwapi nafasi Arsenal kabisa.
.
✍Lakini game ya leo itakua tofauti kidogo nawaona makocha wote wawili Unai na Klopp wakiwapa nafasi wale wachezaji ambao wamekua wakikosa nafasi mara kwa mara!.
.
✍Vikosi vya pili vya timu zote naona vikipata nafasi akina Joe gomez,Martinell,Saka,cylne na wengineo ndio mechi zao hizi kutetea nafasi zao!.
.
✍Ozil asilimia 60% mechi ya leo atakua kiongozi kwa vijana wa Arsenal watakaopewa nafasi dhidi ya Liverpool leo.Ndo muda wa kumprove Wrong Unai naamini atafanya kile wengi tunatarajia ana huwa anavifanya pindi anapopata nafsi zile danger pass tutaziona na zile creativity zake!.
.
.
Prepared by @anode360 Proudly Sponsored by @mcheza_tz @bussi_ntua @tshombee1 #sokaonlineupdates

LIPULI YAFUNGUKA KUHUSU KUKAMATWA WACHEZAJI WAKE

Uongozi wa timu ya Lipuli FC umeshangaa wachezaji wake kushikiliwa na kupigwa na Polisi saa chake kabla ya ‘Wana Paluhengo’ hao kuwakaribisha Polisi Tanzania katika uwanja wa Samora mkoani Iringa.

Tukio hilo lilitokea jana jioni ambapo leo saa 10 jioni Lupuli itaikaribisha Polisi katika uwanja wa Samora.

Mwenyekiti wa timu hiyo, Ayoub Kivyelo amesema jana jioni waliwaita baadhi ya wachezaji wao katika ofisi za klabu hiyo zilizopo uwanja wa Samora lakini baada ya kutoka nje wakakutana na gari ya Polisi ambayo walipigwa na kushikiliwa kwa muda kabla ya kuachiwa huru.

Kivyelo amesema wachezaji Paul Nonga, Seif Karihe na Daruwesh Saliboko ambao. walipigwa wakaachwa lakini Issa Ngoah alipigwa wakaondoka nae kabla ya kumuachia baada ya muda. “Hata hatuelewi sababu ni nini, wamewapiga wachezaji wetu wakawashilia kabla ya kuwaachia lakini mchezaji Issa Ngoah mpaka tukampeleka hospitali usiku,” alisema Kivyelo.

@officiallipulifc @tanfootball @polisitanzaniafootballclub
#wapendasokaupdates

Maradona aendeleza kutoa vichapo vikali

πŸ‘‰ FELIZ CUMPLEAΓ‘OS, EL PIBE DE ORO πŸ’₯.
:
✍🏻 Diego Maradona alijihakikishia kuwa yuko vizuri wakati akiiongiza klabu yake ya Gimnasia La Plata ikiipiga Newell’s Old Boys 4-0 jana usiku.. Mshambuliaji huyo nyota Duniani wa zamani anachukuliwa kama mfalme na watu wengi huko Argentina na ili kuilinda hadhi yake ya kifalme, ndani ya uwanja wameamua kumuwekea kiti cha enzi na hatokaa eneo la benchi maalumu ndani ya uwanja.. πŸ˜‚πŸ˜„πŸ˜„πŸ™ŒπŸ»

✍🏻 Maradona, ambaye alishinda Kombe la Dunia mnamo 1986 na kwa ujumla anachukuliwa kuwa mmoja wa Wachezaji bora kabisa kucheza mchezo wa Soka, alichukua jukumu la kuwa kocha Mkuu kuinoa, Gimnasia katika jiji la La Plata, karibu na nyumbani kwao alikozaliwa Buenos Aires, mnamo mwezi Septemba.


✍🏻 Gimnasia hawajawa na nyakati nzuri zaidi katika Superliga, lakini wameshinda mara mbili tu katika michezo yao 11 msimu huu, wakitoka sare mchezo mmoja na mechi nyingine zoote wakipokea Kipigo… Wapo nafasi ya Pili kutoka chini katika Ligi yenye timu 24..
#Updates #Maradona #DiegoMaradona
@Harunlugoyah

Wachezaji wenye hatari ya kuuzwa ili Barcelona ikamilishe bajeti yake ya msimu

Klabu ya FC Barcelona ilipitisha bajeti mpya ya msimu mnamo October 4, kwa msimu huu wanahitaji kiasi cha Euro millioni – lakini ili kufikia target waliyojiwekea wanahitaji kuuza wachezaji ambao wataweza kuzalisha kiasi cha 124m kabla ya June 30, 2020.
.

Klabu hiyo tayari imeshaanza kufanyia kazi mauzo ya baadhi ya wachezaji na mazungumzo yanaendelea.

Hawa ndio baadhi ya wachezaji wanaotajwa kuwekaa sokoni ili Barca ikamilishe bajeti yake. .
.
. β€’Ivan Rakitic
Kiungo huyu wa Croatia yupo kwenye siku za mwisho za maisha yake ndani ya Camp Nou, alinusurika kuuzwa wakati wa dirisha la kiangazi baaada ya kupoteza nafasi kikosini, lakini sasa huenda dirisha la mwezi January likamuondoa Blaugrana.
Juventus walimhitaji na huenda wakarejea tena lakini pia kuna uwezekani akaenda aidha Inter au Manchester United wenye uhitaji wa kiungo kama Rakitic .
.
.
. β€’ Arturo Vidal

Vidal hajawahi kuwa na nafasi ya kudumu katika kikosi cha Barca na sasa amepoteza zaidi nafasi na hili limezidisha timu zinazomhitaji kuzidi kumtolea macho – wakiongozwa na Inter Milan ambao kocha wao Antonio Conte anamhusudu sana Vidal.
Barcelona wanahitaji kumuuza sasa ili kupata pesa na kuondokan na hatari ya kumpoteza kwa uhamisho huru mwaka 2021. .
.
β€’ Coutinho & Malcom πŸ‡§πŸ‡· .
Wabrazil hawa wawili ni biashara ambazo biashara ambazo zinahitaji ukamilifu tu.
Malcom aliuzwa kwenda Zenit Saint Petersburg kwa ada ya jumla ya 40m euros, lakini mpaka sasa imelipwa kiasi cha 8.2m euros, malipo mengine yataendelea kulingana na mkataba waliokubaliana.
Coutinho yupo kwa mkopo Allianz Arena, The Bavarians wanaweza kumsaini mchezaji huyo kwa ada ya uhamisho wa 120m euros – mpaka sasa ameanza vizuri msimu kiasi cha kuwashawishi vibopa wa Bayern kulipa fedha hizo ili kumsaini kiungo huyo wa Brazil. . .
. β€’ Samuel Umtiti
Alikuwa na msimu bora sana wa 2017/18, lakini msimu uliopita majeruhi yaliharibu sana maendelea ya career yake ndani ya klabu. Barca bado wanamhitaji lakini huenda wakamuuza kutokana tu na majeruhi.
Wachezaji wengine ambao huenda wakauuzwa ni Carles Perez, Moussa Wague na Marc Cucurella.

Design a site like this with WordPress.com
Get started