š£ļø”Bado nina mkataba na Bandari, na nguvu zangu zote nimeziweka huku, nimeshangazwa sana na taarifa za kuhusishwa na Yanga, sinaongea nao.” .
Maneno ya Ben Mwalala aliyehusishwa na kutua Jangwani.
#bakinasisi__ #NjooKwetu #TupoNawePaleUlipo
Adhabu kali zawahusu wachezaji Alliance.

Wachezaji wawili wa Alliance fc ya huko jijini Mwanza wamekumbana na adhabu kwa vitendo walivyovifanya katika mechi ya ligi kuu Tz bara. Kupitia kamati ya nidhamu ya Alliance FC imewapiga faini wachezaji hao waliopewa kadi nyekundu katika mchezo dhidi ya Mbeya City.
Wachezaji hao ni kipa John Mwanda na nahodha Israel Patrick.
.
Mchezo huo ulipigwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Nyamagana, ambapo wachezaji hao walionyesha vitendo visivyo vya kiungwana kwa wenzao na kusababisha mwamuzi Shomari Lawi kuwaonyesha kadi nyekundu kila mmoja.
.
Katika mechi hiyo, Mwanda alionekana kumchezea rafu straika wa Mbeya City, George Chota huku Patrick akionyesha kumshika sehemu nyeti mchezaji Idd Gomba na kusababisha Alliance kumaliza mpambano wakiwa pungufu.
.
Makamu mwenyekiti wa klabu hiyo, Stephano Nyaitati alisema katika kuhakikisha nidhamu inatawala kamati ilikaa juzi na kuamua wachezaji hao kulipa faini kulingana na makosa husika.
.
Alisema Patrick aliamuriwa kulipa faini ya Sh250,000 huku Mwanda akitakiwa kulipa Sh200,000 na hiyo ni kwa mujibu wa kanuni za klabu kwa wachezaji. Pia makamu huyo alisema kuwa wamejipanga kulinda nidhamu kwa wachezaji wao.
.
#bakinasisi__
#TupoNawePaleUlipo
#NjooKwetu
Juventus kukiwasha kwa Locomotiv Moscow
T

MABINGWA wa Serie A, Juventus watakuwa ugenini leo Jumatano usiku kupepetana na Lokomotiv Moscow katika pambano la Ligi Kuu ya Ulaya. Vijana hao wa kocha Maurizio Sarri wanaongoza kundi D kwa pointi saba wakati Lokomotiv wakijivunia pointi tatu katika nafasi ya tatu nyuma ya Atletico Madrid baada ya kujibwaga uwanjani mara tatu.
.
Wenyeji ambao walishindwa na Atletico nyumbani na baadaye Juventus ugenini, watahitaji kushinda mechi ya leo ili kujiongezea matumaini ya kufuzu kutoka katika kundi hili ambalo pia linajumuisha Bayern Leverkusen ya Bundesliga. Wenyeji wangali na uwezo wa kumaliza katika nafasi ya tatu jedwalini, nafasi ambayo itawawezesha kushiriki michuano ya Eropa League, msimu ujao.
.
Vijana hao wa kocha Yuri Semin wataingia uwanjani baada ya mwishoni mwa wiki kutoka sare 1-1 na FC Ufa katika pambano la ligi kuu nchini hapa, wanakoshikilia nafasi ya tatu, pointi tatu tu nyuma ya vinara Zenit St Petersburg. Hata hivyo, wameshinda tu mechi tano kati ya 14 za Ulaya jijini hapa, tatu kati ya nne kwa timu za Italia, rekodi inayowapa mashabiki wao wasiwasi mkubwa.
.
Juventus wanaongoza msimamo wa kundi hilo baada ya kucheza mechi tatu. Walianza kwa sare ya 2-2 na Atletico Madrid kabla kuandikisha ushindi dhidi ya Leverkusen na baadaye Lokomotiv.
.
Katika mkondo wa kwanza, mabao ya Juventus yalifungwa na Paulo Dybal dakika ya 77 na dakika ya 81.
.
Huu ni mwaka wa 20 kwa vigogo hao wa Italia kushiriki hatua ya makundi ya michauno hii, na wametinga hatua ya 16 bora kati ya 19.
.
Robo-fainali Msimu uliopita, Juventus walifuzu kwa hatua ya robo-fainali, lakini kwa mshangao wakabanduliwa na Ajax Amsterdam ya Uholanzi. Hata hivyo, klabu hiyo imepoteza fainali tano za klabu bingwa Ulaya, na hawajashinda taji hilo tangu 1996. Vilevile, nyumbani wanakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Inter Milan kwenye vita vya kuwania ubingwa wa Serie A.
.
Wataingia uwanjani leo baada ya ushindi finyu wa 1-0 dhidi ya Torino katika mechi ya Serie A mwishoni mwa wiki, uliowarejesha kileleni mwa jedwali, mbele ya Inter ambao kwa sasa wanaendelea kuvuma chini ya Antonio Conte aliyekuwa na Chelsea, msimu uliopita.
#bakinasisi__ #NjooKwetu
Gerard Pique ataukosa mchezo dhidi ya Dortmund nyumbani

Gerard Pique ataukosa mchezo dhidi ya Dortmund nyumbani baada ya kuoneshwa kadi ya Njano Jana dhidi ya Slavia Prague
.
Slavia Praha imekuwa timu ya kwanza kupata Clean Sheet katika dimba la Nou Camp katika michuano ya Uefa hatua ya makundi tangu ilipofanya hivyo Benfica Disemba 2012.
.
#bakinasisi__
#NjooKwetu #TupoNawePaleUlipo
Kiungo wa Arsenal, Granit Xhaka amevuliwa Unahodha

āš» Kiungo wa Arsenal, Granit Xhaka amevuliwa Unahodha ndani ya klabu hiyo huku Mshambuliaji wa Kimataifa wa Gabon š¬š¦, Pierre-Emerick Aubameyang akichukua nafasi yake, kocha Mkuu wa The Gunners Unai Emery amethibitisha.
..
āš» Sababu ya Xhaka, 27, kutolewa katika jopo la Manahodha ni lile tukio lake katika mechi ya Premier League iliyotoka kwa sare ya 2-2 dhidi ya Crystal Palace mnamo 27 Oktoba… š£”Nilikuwa na mkutano na yeye na nikamwambia hayumo tena katika kundi la Ma-nahodha, Alikubali uamuzi wangu, Nilihitaji kuchukua uamuzi na sasa imetimia”.. Alisema Emery jana Jumanne.
#PremierLeague #Arsenal
@Harunlugoyah
Nugaz ametimiza ahadi yake ya kupeleka Magodoro 30 ya Chapa GSM

Afisa mhamasishaji wa klabu ya Yanga Sc Antonio Nugaz ametimiza ahadi yake ya kupeleka Magodoro 30 ya Chapa GSM na matofali 500 pamoja na cement mifuko 30 katika shule ya Al Rushdy Sec. School iliyopo Kigamboni
:
Nugaz amesema mdau yeyote anaweza kuwapigia kwa simu Namba 0714 224 800 kwa chochote kama umegusa na hili pia na wewe ukaendelea kuchangia
:
Hongera sana Nugaz @antonionugaz
Mzee wa Cleen Sheet
Yanga yaanza safari kuifuata ndanda

Kikosi cha klabu ya Yanga Sc leo asubuhi kimeanza safari ya kwenda Mjini Mtwara kwa ajili ya maandalizi ya Mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Ndanda Sc.
: Anthony Joshua vs Andy Ruiz Jr. – Kibonge aamua kupunguza mwili. .

Dec. 7
Mwezi mmoja kabla ua pambano la marudiano dhidi ya Anthony Joshua, bingwa wa dunia uzito wa juu Andy Ruiz Jr ameamua kupunguza mwili ili aweze kuwa mwepesi kwenye pambano hilo, amesema mtaalam wa lishe wa bondia huyo. .
Picha kadhaa kutoka kwenye Social media zinaonyesha bondia huyo akionekana mwembamba na sasa imethibitishwa kwamba ni kwasababu ya maandalizi ya pambano ya marejeano vs Joshua litakalofanyika nchini Saudia Arabia mnamo December 7. |
Inaelezwa Andy amebadili mazoezi na pia mlo wake umekuwa maalum kumpa nguvu lakini pia kupunguza mafuta mwilini. “Diet yake inahusisha Samaki, salmon, pasta katika siku za mazoezi ya āsparringā (kupigana). Mara kadhaa huwa anaweza kula chakula chochote anachopenda (cheat day) lakini sio vyakula ambavyo vinaweza kumharibia kabisa. “Lengo ni kumfanya ale chakula ambacho kinamfaa kiafya, ili azidi kuwa mwepesi ulingoni. “Hatuna namba maalum ya uzito tunaotaka – anaweza kupungua kidogo, lakini cha muhimu ni ajihisi mwepesi Hii itamfanya aweze ili iwe rahisi kwake kuchezesha miguu yake ulingoni.ā Ruiz Jr alipimwa na kukutwa na uzito wa 19st 11lbs, alimzidi Joshua wakati walipopigana kwa mara ya kwanza jijini New York mapema mwaka huu. .
|
Kwa upande wa Anthony Joshua inaelezwa hivi sasa amehamishia sana mazoezi kwenye āsparringā – promota wake Eddie Hearn amesema mteja wake amejiandaa vyema ili kuweza kurudisha mataji yake ya IBF, WBA na WBO.

Emerick Aubameyang kutua Real madrid

Taarifa zilizoenea leo hii nikwamba Nahodha mpya wa Arsenal, Pierre Emerick Aubameyang anahitajika katika klabu ya Real Madrid ya Hispania. Aubameyang ana mkataba na Arsenal unaomruhusu kuondoka endapo klabu inayomtaka itatoa kiasi kisichopungua £72M na inaelezwa kuwa Arsenal wapo tayari kumuuza kwa £80M
Aubameyang ameteuliwa leo kuwa nahodha mpya wa Arsenal akitwaa mikoba ya Granit Xhaka aliyevuliwa kitambaa hicho kwa makosa ya utovu wa nidhamu.
#wapendasokaupdates