CLUB AFRICAIN NA YANGA NDUGU! . .bakuli lashika hatamu

Yale tuliyoyashuhudia kwa Yanga kupitisha bakuli kwa mashabiki wa klabu hiyo ili kupata fedha za kujiendesha – yamejitokeza kwa namna nyingine nchini Tunisia.
.
.
Mashabiki kindakindaki wa Club Africain wachangia $450,000 za Kimarekani kwa siku moja (zaidi ya bilioni 1) ili kusaidia kulipa deni la klabu hiyo
:
Mashabiki wa klabu kongwe ya Tunisia ikiwa ni pamoja na shabiki mmoja mwenye ulamavu wa macho ambaye alichagua kutoa fedha ya gharama za dawa anayotumia ili kusaidia timu yake pendwa, kwa ujumla wametoa zaidi ya Dola $450,000 (Pauni 350,000) kwa siku moja wakati wanapambana kuokoa klabu kutoka katika ukata wa kifedha

Club Africain, ambayo ni klabu ya pili kongwe Tunisia na moja ya klabu zinazojulikana barani Afrika, imekatwa pointi sita na kupigwa faini ya kifedha ($6m) kwa sababu ya kutolipa mishahara kwa wachezaji wake wa zamani.

Ili kusaidia klabu ambayo ilianzishwa mwaka 1920, Shirikisho la Soka la Tunisia (FTF) liliunda kamati ya usimamizi wa mgogoro huo ili kuokoa timu kutopata na vikwazo zaidi.

Ilikuwa mwezi Oktoba, FTF ilianzisha akaunti ya benki kwa mashabiki kutoa pesa kusaidia kuondoa deni ambalo linaikabili Club Africain na hadi sasa dola za Kimarekani 600,000 zimekusanywa.

Katika kampeni ya masaa 24 iliyofanyika Junanne, mashabiki wa Club Africain wameonyesha kina cha kujitolea kwao kwa kilabu, ikiwa ni pamoja na mashabiki wazee na watoto ambao walifika na benki listi za malipo ya benki kwenye makao makuu ya klabu hiyo uku wakiwa na shabiki ambaye ni mlemavu wa macho aliyekabidhi akiba yake na klabu ilionyesha heshima kwa kumkabidhi jezi iliyosainiwa na wachezaji wote wa Club Africain.

Hiyo jumla pamoja na michango ya Jumanne inamaanisha klabu ya Africain imefikisha zaidi ya $ 1m kwa deni lote ambalo shirikisho limeweka ikiwa ni $ 6m (bilioni 13.8)

KYLE WALKER AIDAKIA MAN CITY JANA

Beki Wa pembeni Wa klabu Wa Manchester City Kyle Walker Jana usiku alijikuta akivaa gloves na kuwa kipa wakati Manchester city ikitoka sare ya bao 1-1 na Atalanta nchini Italia baada ya kipa namba mbili Claudio Bravo alipotolewa nje kwa kadi nyekundu huku kipa aliyeanza Ederson akiumia wakati Wa mapumziko.

Walker hakufungwa bao lolote akijitahidi pia kuokoa baadhi ya michomo

#wapendasokaupdates

Jina lake halisi ni Oluwafikayomi Oluwadamilola Tomori. .

Jina lake halisi ni Oluwafikayomi Oluwadamilola Tomori na alizaliwa Desemba 19, 1997 katika Mji wa Calgary, Alberta, Canada. Wazazi walikuwa Wanigeria lakini ambao walihamia jijini London, England.
.
Hivyo alipata nafasi ya kuanza maisha yake ya soka katika kikosi cha Chelsea chini ya umri wa miaka minane na kisha kujiunga katika shule yao ya soka. Alikuwa katika kikosi cha Chelsea ambacho kilitwaa mataji ya kombe la vijana la Uefa na FA miaka ya 2015 na 2016.

Mei 11, 2016 Tomori alitajwa katika kikosi cha kwanza cha Chelsea cha wakubwa kwa mara ya kwanza alikaa benchi na wachezaji wenzake wa timu ya vijana Tammy Abraham na Kasey Palmer, katika pambano dhidi dhidi ya Liverpool lililomalizika kwa sare ya 1-1.
.
Mei 15, 2016 Tomori alicheza pambano la kwanza la timu ya wakubwa jezi ya Chelsea katika pambano la mwisho la msimu wa 2015/16 dhidi ya mabingwa Leicester City. Aliingia dakika ya 60 kuchukua nafasi ya Branislav Ivanović.
.
Januari 23, 2017 Tomori alipelekwa kwa mkopo katika klabu ya Ligi Daraja la Kwanza Brighton & Hove Albion kwa ajili ya kumaliza msimu wa 2016–17. Siku tano baadaye alicheza mechi ya kwanza kwa Brighton katika kichapo cha mabao 3-1 ugenini dhidi ya Lincoln ya daraja la nne raundi ya nne ya michuano ya FA. Alicheza mechi ya kwanza ya ligi katika ushindi wa mabao 2-0 ugenini kwa Barnsley, akichukua nafasi ya Anthony Knockaert katika kipindi cha pili.
.
Machi 18, 2017 alianza mechi yake ya kwanza katika kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Leeds United akicheza dakika zote 90.
Apelekwa kwa mkopo Hull City, Derby Agosti 31, 2017, Tomori alijiunga na klabu ya daraja la kwanza ya Hull City kwa mkopo wa msimu mzima. Alicheza mechi yake ya kwanza Septemba 13, 2017 katika kichapo cha mabao 2-1 ugenini dhidi ya Fulham.
.
Bao lake la kwanza kwa Chelsea Septemba 14, 2019 kwa shuti kali la nje ya boksi katika pambano dhidi ya Wolves ambalo walishinda mabao 5-2 ugenini. Kuumia kwa beki, Antonio Rudiger kumemfanya kuaminiwa sana na Lampard.
.
#bakinasisi__ #NjooKwetu #TupoNawePaleUlipo

Je.simba kuendeleza vipigo vikali leo

Simba Vs Tz Prisons
🏟️ Uhuru Stadium
⏱️ 10:00 Jioni
#VPL
.
Simba wapo kileleni mwa msimamo wa ligi wakiwa na alama 21 baada ya kucheza mechi 8, Simba wataingia nakumbukumbu ya kutoa kipigo cha goli 4-0 mechi iliyopita, huku wakiwa wamepoteza mchezo mmoja tu hadi hivi sasa, wakifungwa na Mwadui 1-0. (W W W W W W W L).
.
.
Prisons kwa sasa ipo chini ya aliyewahi kuwa mchezaji wa zamani wa Yanga na Pan African, Mohammed Rishard ‘Adolph’ imecheza mechi tisa mpaka sasa huku ikishinda tatu na kutoa sare michezo sita.
.
Tz Prison ipo nafasi ya tano katika msimamo wa ligi baada ya kufikisha pointi 15 kutokana na ushindi wa bao 1-0 iliopata mchezo wao wa mwisho dhidi ya maafande wenzao JKT Tanzania, hawajapoteza mchezo wowote hadi hivi sasa. (D W D D D W D D W)
.
dondosha comment yako hapo leo nani kulazwa na viatu….???
#bakinasisi__
#TupoNawePaleUlipo
#NjooKwetu

MWINYI ZAHERA ULIKOSEA MWENYEWE

:

Kuna muda macho yetu huhukumu lakini kuna nyakati uhalisia ubaki kuwa kwenye uhalisia wake!!!
:
Mimi binafsi siyo muumini wa aina ya makocha kama ZAHERA, binafsi napenda makocha wanaoongea kwenye touchline, wanaokujiba kwenye mbinu uwanjani na matokeo mazuri uwanjani!!
:
Sipendi kocha aliye rafiki sana na media napenda kocha aliye rafiki sana na pitch na soka safi na matokeo mazuri!!
:
Zahera alikuja kwa mlengo wa kuuonesha umma wa wapenda soka wa Tanzania kwamba yeye anajua kila kitu ila amesahau kwamba kuna watu wanajua zaidi yake na wametulia, Zahera weapon yake kubwa ilikuwa media na huruma za mashabiki ndio maana alikuwa mstari wa mbele kufanya lolote kuhusu mashabiki na media na si kuijenga Yanga kuwa ya ushindani uwanjani!!
:
Yanga iliyoshindwa kushinda hata kwa margin ya 4-0 kwa karibu mwaka na nusu itawezaje kuwa bora na kupata mafanikio?? Character ya tim kubwa na yenye kiu ni pale inapocheza na tim dhaifu kupata margin kubwa, leo Yanga ikicheza na tim za kawaida huoni tofauti kati ya Yanga na tim dhaifu!!
:
Leo Yanga haina uhakika wa kushinda mechi mpaka mpira uishe hii ni hatari kwa afya ya Yanga!!
:
Kocha anakwambia amesajili wachezaji kwa ajili ya ligi kuuu maana yake ili uwe bingwa ni lazima uwe na wachezaji bora au wanaolingana na Simba ambaye nso bingwa mtetezi lakini unajiuliza kweli kati ya wachezaji waliosajiliwa msimu huu ukimuondoa Lamine Moro kuna mchezaji mwingine yupi anayeweza kupata nafasi kwenye kikosi cha Simba??? Hapa inaonesha jinsi kwanza Kocha ameshafeli kwenye attempt ya kwanza kwenye usajili!!
:
Yanga inaingia pre season kocha anakula bata ufaransa ni kweli ilikuwa muda wa likizo lakini kuna changes za ratiba za CAF kwanini kocha asingeona umuhimu wa ratiba zilizo mbele yake?? Hapa ndipo alipofeli attempt yake ya pili!!
:
Kocha anaanza mashindano hajui mchezaji gani atacheza na nani ili kuweza kutengeneza timu ya ushindani?? :
Zahera aliandaa mazingira ya kujifukuzisha kazi kabla hajafukuzwa!!
:
Inaendelea
Prepared by Karim Kondo

MATOKEO YA SOKA JANA +RATIBA YA SOKA LEO :

#VodacomPrimierLeague
FT Mtibwa Sugar 1-0 Mwadui FC
FT Polisi Tanzania 0-1 Mbao FC
FT Coastal Union 0-1 Alliance FC
FT JKT Tanzania 1-0 Mbeya City
FT Namungo FC 2-1 Ruvu Shooting
FT Lipuli FC 5-1 Singida United
:
#UefaChampions League
FT Paris Saint-Germain 1 – 0 Club Brugge
FT Real Madrid 6 – 0 Galatasaray
FT FC Bayern München 2 – 0 Olympiacos
FT FK Crvena Zvezda 0 – 4 Tottenham Hotspur
FT Atalanta 1 – 1 Manchester City
FT Dinamo Zagreb 3 – 3 Shakhtar Donetsk
FT Lokomotiv Moscow 1 – 2 Juventus
FT Bayer Leverkusen 2 – 1 Atletico Madrid
:
#UefaEuropaLeague
FT Vitoria de Guimaraes 1 – 1 Arsenal
:
#WorldCup U-17 – Play-off
FT Japan 0 – 2 Mexico
FT Spain 2 – 1 Senegal
FT Brazil 3 – 2 Chile
FT France 4 – 0 Australia
:
#KenyaPremierLeague
FT Gor Mahia 0 – 1 Mathare United
FT Western Stima 3 – 1 Bandari
:
#MoroccoBotolaPro
FT Hassania Agadir 2 – 1 FAR Rabat
FT MAT Tetouan 1 – 1 Olympic Club de Safi
FT RSB Berkane 2 – 1 Rapide Club Oued Zem
FT Wydad Casablanca 4 – 0 Ittihad Tanger
:
#SouthAfricaPremierLeague
FT Amazulu Durban 2 – 0 Stellenbosch FC
FT Baroka FC 0 – 0 Mamelodi Sundowns FC
FT Cape Town City FC 5 – 3 Polokwane City
FT Chippa United FC 0 – 2 Kaizer Chiefs
:
#VodacomPrimierLeague
16:00 Simba Sc vs Tz Prisons :
#UefaEuropaLeague
20:55 APOEL Nicosia vs Qarabag FK
20:55 F91 Dudelange vs Sevilla
20:55 FC Koebenhavn vs Dynamo Kyiv
20:55 Lugano vs Malmoe FF
20:55 Basel vs Getafe
20:55 FC Krasnodar vs Trabzonspor
20:55 LASK vs PSV Eindhoven
20:55 Rosenborg vs Sporting CP
20:55 CFR Cluj vs Rennes
20:55 Lazio vs Celtic
20:55 Standard Liege vs Eintracht Frankfurt
23:00 Feyenoord vs Young Boys
23:00 Rangers vs FC Porto
23:00 RCD Espanyol vs Ludogorets Razgrad
23:00 Ferencvaros vs CSKA Moscow
23:00 Oleksandriya vs Saint-Etienne
23:00 Wolfsburg vs Gent
23:00 Borussia Mönchengladbach vs Roma
23:00 Wolfsberger AC vs Istanbul Basaksehir
23:00 SC Braga vs Besiktas
23:00 Wolverhampton Wanderers vs Slovan Bratislava
18:50 FC Astana vs AZ Alkmaar
23:00 Manchester United vs Partizan Beograd
:
Prepared @officialchristz
Powered by @bikotanzania

Design a site like this with WordPress.com
Get started