Vita ya kuwania ufungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara imezidi kupamba kushika kasi ya 4G baada ya washambuliaji wawili wa Lipuli, Daruweshi Saliboko na Paul Nonga kufikisha mabao sita wakiwa nyuma kwa mabao mawili kwa kinara Meddie Kagere wa Simba.
.
Kagere anaongoza msimamo wa wafungaji bora akiwa amefunga mabao nane wakati Saliboko na Nonga wote wamefikisha mabao sita kila mmoja. Mabao matatu aliyofunga Saliboko na mawili ya Nonga katika mchezo dhidi ya Singida Utd jumatano ya wiki hii yametosha kuwapaisha wachezaji hao hadi katika nafasi ya pili katika msimamo wa wafungaji na kumkaribia Kagere.
.
Wachezaji wengine wanaofuatia katika chati ya wafungaji ni Athuman Miraj wa Simba, Peter Mapunda (Mbeya City), Yusuf Mhilu (Kagera Sugar) na Gerald Mathias Mdamu wa Mwadui wenye mabao manne kila mmoja.
.
C

omment fupi fupi chapu tupite. Unaionaje kasi hii..??
#bakinasisi__
#TupoNawePaleUlipo
#NjooKwetu





:

:
:

