
Klabu ya soka ya Rufiji United inayoshiriki ligi Daraja la Pili(SDL imetambulisha Jezi zake Mpya mbele ya rais wa zamani wa Tanzania Mh: Daktari Jakaya Mrisho Kikwete siku chache zilizopita
:
Rufiji United ipo chini ya Mbunge wa Rufiji.

Klabu ya soka ya Rufiji United inayoshiriki ligi Daraja la Pili(SDL imetambulisha Jezi zake Mpya mbele ya rais wa zamani wa Tanzania Mh: Daktari Jakaya Mrisho Kikwete siku chache zilizopita
:
Rufiji United ipo chini ya Mbunge wa Rufiji.

Magazeti Michezo Leo
Gazeti la Dimba na Heading kubwa
Kuwa
:
➡klabu ya Yanga Sc yanasa Bonge la Straika
➡Habari Leo Mbwana Samatta aseme kikosi cha Stars kitawafurahisha Mashabiki wote wa stars
➡Nipashe Mkwasa asema hichi ndicho kinachoitesa Yanga Sc :
Soma kwa Undani upate Nini kimejiri katika magazeti leo










1: WHAT A MATCH 🙌 As usual, Liver Vs City hua ni mechi ya Klopp Vs Guardiola. Anaenasa kwenye mtego wa mbinu za mwenzake, anapotea mazima
.
.
2: Guardiola aliimisi sana miguu ya Ederson kuliko mikono yake. Bravo hakua active kwenye kuutengeneza mchezo wa City kutokea chini
.
.
3: Trent Alexander-Arnold na Robertson (kwa mtazamo wangu) hawa ndio wachezaji muhimu kwenye plan ya Klopp kuliko Mane, Salah na Firminho. Those kids ni machine aisee🙌 Nilimuonea huruma sana Walker alivyokua akilazimishwa kufanya anachowafanyiaga wenzake.
4: Sergio Kun Aguero😔 Mchezaji mkubwa asiekua na madhara Anfield. Mechi 10 bila bao🤔 presha hii kwa kiasi fulani ilimpotezea umakini kwenye eneo la mwisho.
5: Fabinho & Wijnaldum🙌 wakiwa na mpira unamuona Mbrazil na Mholanzi.. bila mpira unamuona Mruguay na Mjerumani👐 Akili kubwa iliyojazwa upepo kwenye mapafu yao.. Wanakimbia muda wote🙌 .
.
6: Raheem Sterling👐 Katika presha ile ya Anfield, bado ameendelea kua mchezaji mwenye madhara kwa City. Ni mawinga wachache sana duniani wanaoweza kushinda vita dhidi ya Trent Alexander Arnold
.
.
7: Kama kuna kitu cha maana Klopp alikifanya pale Anfield basi ni ile sub ya Gomes. Trent akasogea juu kuanza kumzuia Angelino, mchezaji wa kawaida kwenye line up ya City lakini alikuwa na hatari kubwa kwenye mikimbio yake.
8: Fernandinho. Siku zinakwenda mwishoni. Dhidi ya wapinzani wenye presha, nguvu, kasi kama Liver, mambo yanaonekana kuwa mazito kwake
.
.
9: Nilipenda Spirit ya Lovren🙌 Angalau alimpunguzia majumuku mengi VVD. Kadri presha ilivyozidi kua kubwa, ndio alizidi kuingia mchezoni.
10: Pointi 8 kileleni, lakini nafikiri Klopp anatakiwa kuomba kikosi chake kisikumbwe na majeraha kabla ya kuanza kufikiria ubingwa. Sioni Plan B yake ikiwa na maana sana.
Nb: Refa nae ni binadamu na VAR ni mashine kama zilivyo mashine nyingine..😀

Haijalishi kuwa jiji kubwa kabisa ndani ya Equatorial Guinea linaitwa BATA. Hapa Bongo kwani hatuli Bata?
Haijalishi kwamba kwenye jiji hilo ndipo ulipojengwa uwanja mkubwa kabisa nchini humo, Estadio de Bata wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 35,700 tu. Kwetu haijalishi chochote.. Hako ka Uwanja kao ni nusu tu ya uwanja wetu wa Taifa ‘unaomeza’ mashabiki 60,000. Sasa kama tunaujaza Uwanja wetu tunashindwaje kuwafunga?
Tumewazidi hao Guinea kila kitu…
Wakija wataduwazwa na ukubwa wa uwanja, watashangaa idadi ya watu (60,000) watakaoujaza uwanja wa Taifa.
Watapagawishwa na #Vitochi vyetu. Sasa sikia, mimi na wewe tukaujaze Uwanja wa Taifa na Vitochi vyetu.. Pointi tatu hizi ni muhimu kwetu.. HAWATOKI.. Kwa pamoja tunasema AFCON 2021 TWEN’ZETU TENA
#afcon2021twenzetutena
@waandamizi @tanfootball @taifastars_
Kiungo wa kati wa Chelsea na Ufaransa N’Golo Kante, mwenye umri wa miaka 28, amekana taarifa zinanazomuhusisha na kuhamia katika klabu ya Real Madrid na anasema kuwa anaweza kumalizia taaluma yake ya soka katika Stamford Bridge.
.
Kwa kweli, natarajia kumaliza kazi yangu Chelsea.” alisema Kante akihojiwa katika mahojihano na “Telefoot”.
.
🗣️”Leo nipo na Chelsea hadi 2023. Kwa hiyo kichwani kwangu, natumaini kuendelea kuwa na misimu mizuri na Chelsea hadi 2023.” .
.
Alipoulizwa kuhusu tetesi zinazo muhusu kuhamia Real Madrid, majibu ya Kante yalikuwa rahisi tu: 🗣️ “Hapana, sio kweli”
.
#bakinasisi__
#TupoNawePaleUlipo
#NjooKwetu

Manchester United inaweza kushawishika kujaribu kumrejesha tena mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic katika Old Trafford. .
.
Ibrahimovic mwenye umri wa miaka 38- -mchezaji wa kimataifa wa Sweden atakuwa huru kutokana na kwamba mkataba wake na klabu ya ligi ya MLS – LA Galaxy unakaribia kumalizika.
(TuttoMercatoWeb, via Mail)
#bakinasisi__
#NjooKwetu #TupoNawePaleUlipo

✍ Dimitri Payet ndiye mchezaji wa kwanza wa Marseille kufunga mabao 2 dhidi ya Lyon kwenye mechi ya Ligue 1. Tangu Andres-Pierre Gignac afanye hivo; Mei 4, 2014.
#Ligue1OnStartimes
#StarTimesOn

Goli lake la jana vs City, Limemfanya Mohamed Salah 🇪🇬 kumfikia Yaya Toure katika nafasi ya 5 kwenye listi ya wafungaji wa kiafrika wenye magoli mengi zaidi katika Historia ya Premier League.
.
.
🇨🇮 Drogba (104)
🇹🇬 Adebayor (97)
🇳🇬 Yakubu (95)
🇸🇳 Mané (72)
🇪🇬 Salah (62)
🇨🇮 Yaya (62)
.
.
Kwa kasi hii Salah mpaka anaondoka EPL atakuwa nafasi ya ngapi?

Mchezaji wa Simba @shomari_12_kapombe ni miongoni mwa wachezaji wachache wanaoweza kucheza nafasi nyingi uwanjani na kutekeleza majukumu ipasavyo.
Kwa sasa anacheza sana eneo la ulinzi (kulia) lakini anauwezo mkubwa wa kusaidia kushambilia akitokea pembeni-kulia. Anaweza pia kucheza kama beki wa katikati na kiungo wa kati na amewahi kucheza mara kadhaa.
•
“Nilianza maisha ya soka kama mchezaji wa nafasi za mbele, nikiwa timu ya U14 nilikuwa nacheza kama mshambuliaji mpaka nakwenda U17 bado nilikuwa nacheza nafasi ya ushambuliaji.”
•
“Kuna mchezaji mmoja (alikuwa nahodha wetu) aliondoka kwa hiyo kocha akaanza kujaribu kunivuta nicheze eneo la midfield.”
•
“Mazoezi yalikuwa yanaanza saa 9 kocha akawa ananiambia nifike uwanjani saa 8 nilikuwa nafika saa 8 ananifundisha na vitu vingine ananiandikia, vitu hivyo hadi leo vinanisaidia.”
Kubwa katika Magazeti ya Leo ni Story ya Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars imeingia kambini tayari kwa maandalizi ya mchezo wa Kufuzu Afcon Mwaka 2021 dhidi ya Equatorial Guinea.
Yasome yote kwa Undani Mtu wangu








