KOCHA YANGA ADAI KULIKUWA NA HARUFU ISIYOFAA VYUMBANI

Kocha wa Klabu ya Yanga, Luc Eymael, amesema kuwa kulikuwa na harufu kali na isiyoeleweka katika vyumba vyao vya kubadilishia nguo juzi Jumatano, Februari 6, 2020, katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam wakati mechi yao ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Lipuli FC.

Yanga walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Lipuli, mabao ya Yanga yakifungwa na Mapinduzi Balama dakika ya 14 pamoja na Bernard Morrison dakika ya 31 huku bao la kufutia machozi la Lipuli likifungwa na David Mwassa dakika ya 58.

“Nimeona kipindi cha kwanza kizuri cha Yanga, tulipaswa kufunga magoli matatu au manne…..” alisema Luc.

Aidha, Kocha wa Lipuli Julio Ellieza alisema; “Wametunyima goli dhahiri shahiri, mpira kipa kadakia ndani…. mwamuzi kautoa kuwa kona.”

“Tumefanya makosa, tumeadhibiwa, tunakubali tumefungwa,” alisema Nahodha wa Lipuli FC, Paul Nonga na kuongeza kuwa mpango wao wa kipindi cha kwanza ulifeli ndiyo maana wakafungwa.

Yanga sasa imefikisha pointi 34 baada ya kucheza mechi 17 huku Lipuli ikisaliwa na pointi zake 25 baada ya kucheza mechi 19.

Visit website

ZENEDINE ZIDANE NA N’GOLO KANTE REAL MADRID,ISCO NA LAMPARD CHELSEA

Kwa mujibu wa EL DESMAQURE imeripoti kuwa kocha wa REAL Madrid MFARANSA ZIZOU AMeitaka bodi inayoshughulikia usajili Real Madrid kumsajili mkata umeme KANTE MAJIRA YA KIANGAZI
Kwa mujibu wa EL imefafanua kuwa ZIDANE anahitaji kumjumuisha kiungo mshambuliaji ISCO katika deal hilo ili kumsana KANTE KUtoka CHELSEA

Walianza Kwa THIBAUT
Wakafata Kwa HAZARD
Wakamtoa KOVACIC
Sasa ni…………………watafanikiwa?

Paul John Nonga kucheza ligikuu malaysia

All the best Caption @paulnonga.13

Nahodha wa klabu ya Lipuli fc Paul John Nonga anatarajia kuondoka nchini muda wowote kuanzia sasa kuelekea nchini Malaysia kwaajili ya kuitumikia moja ya klabu inayoshiriki ligi kuu ya nchini humo

Taarifa kamili juu ya timu gani ataichezea itakujia hapa hapa

Powered by @sports_lady_tz
#dailysporttz

Barcelona wametenga kitita cha pauni milioni 4 kwa kipa wa Brighton

Barcelona wametenga kitita cha pauni milioni 4 kwa kipa wa Brighton mwenye umri wa miaka 18 Carl Rushworth, (Mirror)


Barca wanaripotiwa kutuma mascout mara mbili kumtazama kijana huyo ambae anaonekana kuwavutia.
Rushworth pia anacheza timu ya taifa ya England chini ya umri wa miaka19

.

Kwa Mara ya kwanza katika miaka 65 sasa Real Madrid na Barcelona zote zimetolewa Copa Del Rey

Kwa Mara ya kwanza katika miaka 65 sasa Real Madrid na Barcelona zote zimetolewa katika mashindano ya Copa Del Rey baada ya timu zote mbili kufungwa katika mechi zao za Jana.

Real Madrid ikiwa nyumbani ilifungwa bao 4-3 na Real Sociedad huku Barcelona wakifungwa bao 1-0 na Athletico Bilbao
#wapendasokaupdates

Design a site like this with WordPress.com
Get started