Maula.yuko fiti….nani.kukaa goloni

Mlinda lango namba moja wa Simba Aishi Manula amepona majeraha yaliyokuwa yakimsumbua na juzi alianza mazoezi ya kikosi cha kwanza Manula alipata majeraha akiwa kambini nchini Afrika Kusini, majeraha ambayo yalimfanya akose mechi za Stars michuano ya CHAN dhidhi ya Kenya Daktari wa Simba Yassin Gembe amesema mlinda lango huo pamoja na kiungo Ibrahim Ajib …

Shiboub…kawa habari ya mjini kwa sasa

Utawaambia nini mashabiki wa Simba kama kiungo wao Msudan Sharif Shiboub, yuko kwenye kikosi cha kwanza akishika dimba la katikati. Huduma anayoitoa tangu ametua klabuni hapo inawapa mzuka na sasa mabao yake mawili kwenye ushindi wa 4-2 dhidi ya Azam, ndio umewafanya kushangilia kila anaposhika mpira. Kiwango chake kwa sasa kimekuwa mjadala mkubwa na baadhi …

Niyonzima asema hakuna timu yakuifunga simba tanzania

Kiungo wa AS Kigali Haruna Niyonzima amesema anaamini Simba itaifunga UD Songo Jumapili na kusonga mbele hatua inayofuata michuano ya ligi ya mabingwa harani Afrika Niyonzima aliyetembelea mazoezi ya Simba leo, amesema msimu uliopita walijiwekea malengo kuwa hakuna kupoteza mchezo nyumbani “Sisi msimu uliopita tulijiwekea malengo kuwa hakuna kufungwa mchezo wowote nyumbani na tulifanikiwa,” amesema …

Tazama.viingilio vya UD songo

Uongozi wa klabu ya Simba umeweka hadharani viingilio vya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya UD Songo ambao utapigwa Jumapili kwenye uwanja wa Taifa Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara ametaja viingilio hivyo; Mzunguuko Tsh 5,000/- VIP B na C Tsh 15,000/- VIP A Tsh 30,000/- Platinum Tsh 100,000/- Platinum Plus Tsh 150,000/- …

Manara asema yeye ndiye msemaji wa simba

Afisa Habari wa Simba Haji Manara amesema hawezi kukaa katika kiti hicho milele na kwamba itafika siku ataondoka na mwingine atakikalia Hata hivyo amewataka mashabiki wa Simba na wadau wote watambue hadi sasa yeye bado ndiye msemaji wa klabu hiyo hadi hapo itakapotangazwa tofauti Haji amesema hakuna tatizo katika klabu ya Simba Alikuwa akijibu swali …

Watuhumiwa watano wasakwa..tukio la kutekwa MO

Upande wa Mashtaka katika kesi ya kutekwa kwa mfanyabiashara Mohamed Dewji ‘Mo’ umedai kuwa bado wanaendelea kuwatafuta watuhumiwa watano ili kuunganishwa katika kesi hiyo. Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai hayo mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakalima na wanaendelea kuwatafuta watuhumiwa hao watano raia wa Msumbiji …

Mchezo wa simba vs UD Songo .kupigwa saa kumi.jiono

Uongozi wa klabu ya Simba umepanga muda wa mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya UD Songo Mchezo huo utapigwa Jumapili August 25 saa 10 jioni Msemaji wa Simba Haji Manara amewataka mashabiki kuendeleza utamaduni wa kuiunga mkono timu yao kwenye michuano hiyo kwa kujaza uwanja siku ya Jumapili “Kwetu mashabiki sio mchezaji wa …

Kahata atwaa tuzo kenya

Kiungo wa Simba Francis Kahata ameshinda tuzo wa kiungo bora wa ligi kuu ya Kenya msimu wa 2018/19 wakati akiitumikia Gor Mahia Kahata alitwaa tuzo hiyo msimu wa 2017/18 pia Kiungo huyo anayekipiga kwenye timu ya Taifa ya Kenya, ameanza vyema maisha yake kunako klabu ya Simba ambapo mwishoni mwa wiki alifunga moja ya mabao …

Bocco kufanyiwa vipimo zaidi

Nahodha wa Simba John Bocco amefanyiwa uchunguzi zaidi kubaini ukubwa wa jeraha lake alilopata kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam Fc mwishoni mwa wiki Bocco aliumia kwenye mchezo huo baada ya kugongana na Frank Domayo kwenye dakika ya 22 na nafasi yake kuchukuliwa na Clatous Chama Daktari wa Simba Yassin Gembe alisema …

Simba kuweka hadharani uongozi mpya..leo

Uongozi wa klabu ya Simba leo utazungumza na wanahabari katika mkutano utakaofanyika Serena Hotel jijini Dar es salaam Pamoja na mambo mengine, inaelezwa klabu ya Simba huenda itawatambulisha rasmi wafanyakazi wapya wanaojiunga na timu hiyo kwenye nafasi mbalimbali Kwenye Mkutano huo Simba huenda ikamtangaza rasmi CEO mpya ambapo Senzo Mazingisa kutoka Afrika Kusini ndiye anayezungumzwa …

Design a site like this with WordPress.com
Get started