
#VplPreview | Simba Vs Ndanda
Kwenye mechi 13 walizocheza msimu huu, Ndanda ameshinda mechi 1, sare 5 na vichapo 7.
Ni siku 58 zimepita tangu walipopata ushindi wao pekee mpaka sasa, mabao 2-0 dhidi ya Ruvu Shooting
Mechi zao 5 za mwisho, wamefungwa 4, wamepata sare 1 (Ugenini Vs Kagera Sugar 0-0)
Ndanda ni timu iliyosheheni wachezaji wazoefu wa Ligi, lakini hawana muunganiko mzuri kama timu. Kukosa kocha wa uhakika imeendelea kua changamoto kubwa kwao.
Leo wanacheza na @simbasctanzania .. Kocha wa Lipuli aliwaita ‘Mnyama’.. Pamoja na heshima hiyo, mwisho wa dakika 90, akachezea 4-0🙌😀
.
.
Simba ndio vinara wa Ligi, mechi zao 5 za mwisho, wamepata sare 1 tu, wameua 4
.
.
Katika ushindi huo wa mechi 4, wamefunga mabao 13. Idadi ya mabao ambayo Ndanda amefungwa mpaka sasa msimu huu, kwenye mechi zake 13🤔
Simba ni imara sana katikati ya kiwanja. Wana utajiri wa viungo wanaompa jeuri kocha kufanya rotation
.
.
Simba imekua ikipata mabao yake katika maeneo matatu, mastraika, viungo na mawinga.. Inahitaji timu imara sana kuwalinda kwa dakika 90
Utabiri …….❓