Mchezaji huyo wa zamani wa Liverpool mwenye miaka 29 amewasili nchini Uturuki ili kukamilisha usajili wake katika klabu hiyo ikiwa ni baada ya kuachiwa huru na Liverpool
–
Liverpool ilimuachia huru katika kipindi cha majira ya joto cha usajili mwaka huu, ikiwa ni baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka 6 na kufunga magoli 67 katika michezo 160
–
Mshambuliaji huyo wa zamani wa timu ya Taifa ya England alianza kucheza soka la kulipwa katika timu ya Manchester City na baadaye kujiunga Chelsea mwaka 2009