Aussems awaomba mashabiki kuja kuiunga simba mkono

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amewataka mashabiki kuwaunga mkono ili kuhakikisha wanatetea taji la ligi kuu

Akizungumza katika mazoezi yaliyofanyika jana uwanja wa Gymkhana, Aussems alisema anajuwa huu ni wakati mgumu kwa kila Mwanasimba baada ya kutolewa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa

Hata hivyo hawapaswi kuruhusu matokeo hayo yavuruge mipango mingine waliyojiwekea ambayo ni kutwaa taji la ligi kuu na FA

“Najua mashabiki wanavyojisikia, ni hali ambayo pia imetukumba sisi benchi la ufundi pamoja na wachezaji,” alisema

“Tuliwapa wachezaji mapumziko ya siku moja ili waweze kurejea katika hali ya kawaida”

“Tumesahau matokeo hayo, sasa tunawajibu wa kukamilisha malengo yetu ya kutwaa mataji hayo mawili, tuna kikosi imara, tutaweza kufanikisha”

“Muhimu ni kwa mashabiki wetu kuwa nasi, wakati huu mgumu, wasituache, waendelee kutuunga mkono”

Leo alhamis Simba itashuka kwenye uwanja wa Uhuru kuchuana na JKT Tanzania katika mchezo wa kwanza wa ligi kuu msimu huu

Ivan Rakitic. kujiunga na Juventus kwa mkopo

– Kiungo wa kati wa FC Barcelona, Ivan Rakitic anatarajia kujiunga na Juventus kwa mkopo wa mwaka mmoja na kipengele cha kumnunua Baada ya mkopo kumalizika!.
..
– Juventus walikuwa wamewapa Barça Kiungo wao, Emre Can kama sehemu ya mpango wa kubadilishana lakini Barca hawakuvutiwa na kumchukua Kiungo huyo wa Kimataifa wa Ujerumani.
.
– Maamuzi sasa yako mikononi mwa Rakitic kwani lazima aamue kuhama au kubakia Barça na kupigania dakika za kucheza, kwani tayari ameambiwa atakuwa Mchezaji wa Akiba ndani ya Klabu hiyo!..
#fcbarcelona #LaligaUpdates #Juventus
@Sokawaytz

@habarizamichezo

Timu zilizoshiriki mara nyingi hatua ya makundi klabu bingwa africa

Hizi nizo timu ambazo zimeshiriki Mara nyingi Zaidi Katika hatua ya Makundi ya Klabu Bingwa Afrika tangu 1997..
:
Al Ahly 🇪🇬 16
Esperance 🇹🇳 16
ASEC Mimosas 🇨🇮 11
TP Mazembe 🇨🇩 10
Zamalek 🇪🇬 9
Etoile du Sahel 🇹🇳 8
Enyimba 🇳🇬 7
Al-Hilal 🇸🇩 7
Mamelodi Sundowns 🇿🇦 6
Raja Casablanca 🇲🇦 6
Wydad Casablanca 🇲🇦 5
USMA🇩🇿 5

#CAFCL#TotalCAFCL#CAFCLUpdates

Zlatan Ibrahimovic– bado niko vizuri kucheza ligi.kuu england

– Zlatan Ibrahimovic amesema Kuwa anafikiria bado yuko vizuri kucheza kwenye Ligi Kuu ya Uingereza, na kwa utani akasema kwamba Manchester United kama inamtaka inajua yuko wapi, wanaweza Kwenda kumsajili tena.. 😁
:
– Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 alifunga mara mbili kwenye game ya El Tràfico derby wakati timu yake ya LA Galaxy ikitoka sare ya 3-3 na mpinzani wao Los Angeles FC katika pambano la ligi kuu ya Marekani “MLS”.
.
– Magoli hayo mawili yamemfanya kufikisha mabao 22 katika michezo yote ya ligi msimu huu – pamoja na magoli sita kwenye michezo mitatu iliyopita.. anashika nafasi ya Pili Katika ufungaji, kinara Ni mtani wake na mpinzani wake mkubwa huko Marekani, Si mwingine Ni Carlos Vela akifunga Magoli 27 Mpaka Sasa Akiwa na Los Angeles FC… Zlatan Ibrahimovic raia wa Sweden anaamini fomu yake ya hivi sasa inaonyesha wazi angeshindana tena kwa kiwango cha juu huko England…Ibrahimovic alitumia misimu miwili huko Old Trafford kati ya mwaka 2016 na 2018 na alifunga mara 29 katika michezo 53..
#Updates #MLS
@Sokawaytz

KIKOSI CHA YANGA SC HII LEO DHIDI YA RUVU SHOOTING.

1. Faruk Shikhalo
2. Mustafa Selemani
3. Ally Mtoni Sonso
4. Kelvin Yondani
5. Lamine Moro
6. Papy Tshishimbi
7. Juma Balinya
8. Feisal Salim
9. David Molinga
10. Sadney Urikhob
11. Patrick Sibomana

AKIBA.
– Metacha Mnata
– Ally Ally
– Muharami Issa
– Mapinduzi Balama
– Mohamed Issa Banka
– Mrisho Ngassa “Anko”.
– Mybin Kalengo
:
✍️ Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania BARA, Wananchi Yanga SC watakuwa na Kibarua Cha kuwaalika Wanajeshi wa Ruvu Shooting Wazee wa “Noto” Jioni ya Leo ndani ya Uwanja wa Uhuru DSM!.
#VPLUpdates🇹🇿 #YangaSC
@Sokawaytz

Zahera atoa tahadhari kwa wachezaji wake

– Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera amewapa tahadhari wachezaji wake wapya waliosajiliwa msimu huu kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania bara VPL… Yanga iko nyumbani katika Uwanja wa Uhuru hii leo kucheza na Ruvu Shooting, kwenye mchezo wao wa kwanza wa ligi.
.
– Kuelekea mchezo huo, kocha Zahera amesema amewaambia wachezaji wake wapya kutodharau mechi yoyote, huku akisisitiza kuwa wachezaji wa Kimataifa ambao hawakucheza mechi za Klabu Bingwa Afrika kwa sababu ya vibali, wako fiti kucheza mechi za ligi.
.
🗣️ “Nimewaambia wachezaji wote wapya kwamba hakuna hata siku moja Yanga inacheza mechi nyepesi, mechi zote ni ngumu”, amesema kocha Zahera.
🗣️ “Wachezaji wote ambao hawakupata leseni za kucheza mechi za CAF wote watakuwa na nafasi ya kucheza ligi. Wachezaji wote wako vizuri”, ameongeza Papa Zahera!.
#VPLUpdates🇹🇿 #yangasc

Design a site like this with WordPress.com
Get started